Picha sita zinazoonyesha mabadiliko ya hali ya anga

Gundua ni kwa nini hali ya anga ya dunia inabadilika huku viongozi wa dunia wakikutana mjini Paris ili kujadili mpango wa kukabiliana na kuongezeka kwa viwango vya joto

Je, tatizo ni nini?

Viwango vya joto vinazidi kuongezeka duniani

Viwango vya kawaida vya joto duninia vimeongezeka kwa 1.4F katka kipindi cha miaka 100 iliopita.Miaka 13 kati ya 14 ilirekodiwa katika karne ya 21,huku mwaka 2015

Miaka inavyolinganishwa na wastani wa karne ya 20

Miaka 10 yenye joto zaidi

Miaka 10 yeneye baridi zaidi

Viwango vya joto vya kawaida karne ya 20

Joto jingi

Baridi nyingi

Duru:NOAA

Kwa nini hili linafanyika?

Gesi chafu,hususan hewa mkaa

Wanasayansi wanaamini kwamba gesi inayotolewa katika viwanda na kilimo huongezea athari za hewa chafu pamoja na vile anga ya dunia inavyoshika baadhi ya nishati kutoka kwa jua.

Mienendo ya binaadamu kama vile uchomaji wa makaa,mafuta,gesi inaongeza viwango vya hewa mkaa,ambayo ndio gesi chfu inayosababisha kuongezeka kwa viwango vya joto duniani.Misitu inayofyonza gesi hiyo pia imeanza kukatwa

Ongezeko la hewa mkaa katika anga ya dunia ni ya kiwango cha juu ikilinganishwa na miaka 800,000 iliopita na ilifikia kiwango cha juu zaidi mnamo mwezi Mei mwaka huu

Viwango vya hewa mkaa kila mwezi

Data kutoka kwa watafiti wa Mauna Loa

Je,athari zake ni zipi?

Kuyeyuka kwa barafu katika bahari ya Arctic

Kupungua kwa barafu kuanzia mwaka 1980 ni sawa na ukubwa wa taifa la Uingereza

tangu mwaka 1900,viwango vya maji baharini vimeongezeka kwa sentimita 19 duniani.Viwango vya kupanda kwa maji baharini vimeongezeka katika miongo ya hivi karibuni,na kuviweka baadhi ya visiwa na mataifa yalio chini katika hatari kubwa.

Ongezeko la barafu kaskazini ni thibtisho kubwa la viwango hivyo

Kiwango cha barafu katika bahari ya Arctic kinazidi kupungua kwa sababu ya kuongezeka kwa joto na hivyo kuchangia ongezeko la maji baharini

Kupungua kwa barafu kuanzia mwaka 1980 ni sawa na ukubwa wa taifa la Uingereza

1980

1985

1990

1995

2000

2005

2010

2015

Canada
Greenland
Urusi
Uingereza
Marekani
Median (1981-2010)
Barafu ya baharini kiwango cha chini zaidi

Kiwango cha barafu katika bahari ya Arctic :1980, Kilomita milioni 7.8 mraba. 2015, Kilomita milioni 4.6 mraba

Area chart showing the decline in sea ice from 1980 to 2015

Duru:Kituo cha kitaifa cha theluji na barafu

Je, hatua hii inamaanisha nini katika siku za usoni?

Vipimo vya juu vya joto na hali mbaya ya hewa

Kiwango cha athari hakijulikani

Mabadiliko hayo yana uwezo wa kusababisha uhaba wa maji safi,kusababisha mabadiliko makubwa katia uzalishaji wa chakula na kusababisha madhara makubwa wakati wa mafuriko,vimbunga,joto na ukame

Hii ni kwa sababu mabadiliko ya hali ya anga yanatarajiwa kuongeza viwango vya joto lakini hatahivyo huwezi kuhusisha yote haya na kupanda kwa viwango vya joto

Vipimo vya joto vilivyotabiriwa [1986-2005 hadi 2081-2100

iwapo viwango vya gesi chafu vitaongezeka kati ya miaka ya 2010-2020 na baadaye kushuka haraka

Iwapo viwango vya gesi chafu vitaongezeka karne yote ya 21

Duru:Jopo la kimataifa la mabadiliko ya hali ya anga-Ripoti ya tano[AR5]

Nini kinaweza kufanyika?

Mataifa 10 yanayoongoza kwa kutoa gesi chafu duniani

Mataifa hayo yanajumlisha 70% ya gesi yote chafu

Uchina 24%
Marekani 12%
Muungano wa Ulaya 9%
India 6%
Brazil 6%
Urusi 5%
Japan 3%
Canada 2%
DR Congo 1.5%
Indonesia 1.5%

Duru: Taarifa fupi ya Kaboni, Takwimu hizi ni za mwaka 2012

Kuzuia athari

Mataifa 146 yametoa mipango yake ya kutaka kukabiliana na hewa chafu ambayo inatarajiwa kuweka makubaliano ya pamoja kuhusu mabadiliko ya hali ya anga

Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa hewa chafu inayotolewa imesababisha kupanda kwa vipimo vya joto kwa 2.7C ju ya viwango vya viwanda kufikia mwaka 2100

Wanasayansi wamebaini kwamba iwapo vipimo vya joto vitaongezeka na kupita 2C, hali hiyo itasababisha hali mbaya ya anga ambayo itaathiri mataifa yalio na umasikini duniani

Viwango vya joto vya kawaida ifikiapo mwaka 2100

Iwapo mataifa hayatachukua hatua
4.5
Kutokana na sera zilizopo
3.6
Kulingana na ahadi za Paris
2.7
2C

Duru:Wanaofuatilia maswala ya mabadiliko ya hali ya anga,data iliofanyiwa utafiti na wachanganuzi wa hali ya anga ,ECOFYS,Taasisi ya hali mpya ya anga na taasisi ya Postdam kuhusu Utafiti wa athari za hali ya anga

Wahusika

imebuniwa na Emily Maguire, na kutengezwa na Steven Connor na Punit Shah.Imeandikwa na kuzalishwa na Nassos Stylianou na Paul Rincon

Share this story about sharing

email share facebook share twitter share linked in share