bbc.co.uk navigation

Wiji ya BBC Swahili

Wiji ya BBC Swahili ni nini?

Wiji zinawezesha yaliyomo katika tovuti kutumiwa na tovuti nyingine, au kuonekana katika desktop ya kompyuta yako.

Wiji ya BBC Swahili inakuwezesha kuonyesha taarifa za BBC Swahili, pamoja na sikizi na video kwenye tovuti au blogu yako.

Kwanini ninaweza kuhitaji Wiji ya BBC Swahili?

Kwa kutumia Wiji ya Swahili, unaweza kufikisha habari mpya kutoka kote duniani mpaka moja kwa moja kwenye tovuti yako. Ni njia rahisi ya kuwasilisha taarifa muhimu bila gharama.

Ninawezaje kusanikisha Wiji ya BBC Swahili?

Nakili na bandika msimbo hapo chini kwenye mwambaa upande, au sehemu nyingine ya blogu ya tovuti.

Matoleo ya ziada ya wiji yanapatikana kwa iGoogle, Windows Vista Sidebar, Netvibes, Mac Dashboard na WordPress, mengineyo yatapatikana hivi karibuni.

Bofya Ukitaka kuweka wiji katika maeneo mengine tafadhali bofya hapa

Sifa za Wiji ya BBC Swahili

Habari Mpya


Bofya mwambaa wa "Maudhui" kuona aina za maudhui yaliyopo. Watumiaji wanaweza kuchagua maudhui wayapendayo kutoka katika orodha.

Tafuta tovuti ya BBC Swahili
Watumiaji wa tovuti yake wanaweza kutumia wiji kutafuta habari za BBC Swahili.

Andika neno au msemo katika kisanduku cha tafuta na wiji moja kwa moja itakuonyesha matokeo yake.

Jipatie wiji hii
Watumiaji wa tovuti yako wanaweza kupata wiji kwa tovuti au blogu zao kwa kubofya kitufe chenye alama ya +.
Hii inaonyesha msimbo wa kusanifisha wiji.

Chaguo

Haya ni baadhi ya machaguo kwa watumiaji wako. Ukibadilisha utaathiri jinsi wiji itakavyoonekana kwenye tovuti yako.

Chagua chaguo mlisho msingi
Chagua kategoria ya maudhui inayoonekana kwanza wakati wiji inapofunguka.

Ficha muhtasari
Tiki kisanduku kuonyesha vichwa vya habari pekee, lakini si muhtasari wa kila taarifa.

Ficha vijipicha
Tiki kisanduku kuficha picha katika orodha ya taarifa.

USAIDIZI

Bofya kitufe cha alama ya kuuliza kwenda ukurasa wa usaidizi.

MWITIKO NA MASWALI

Tungependa kufahamu mawazo yako. Tafadhali tueleze umependezwa na yapi na kipi kirekebishwe.

Wasiliana Nasi

* Inaashiria uga wa lazima.

(Usizidishe herufi 500)

KANUNI NA MASHARTI YA WIJI

Kwa kusanikisha programu-tumizi ("Wiji ya BBC Swahili") na kuitumia kuonyesha Maudhui ya BBC Swahili unakubaliana na kanuni zilizobainishwa hapo chini.

1. Leseni


1.1 BBC inakupatia leseni isiyo ya kipekee kutumia Wiji ya BBC World Service kuonyesha maudhui ya BBC World Service pekee.

1.2 Haki zote ikiwa ni pamoja na haki za uvumbuzi katika Wiji ya BBC World Service na maudhui ya BBC World Service yanasalia kuwa mali ya BBC.

2.Matumizi ya BBC World Service na Maudhui ya BBC


2.2 Wiji ya BBC World Service ni kwa matumizi yasiyo ya kibiashara pekee.
.
2.3 Hauruhusiwi kunakili, kuchapisha upya, kuhariri, kubadilisha au kuongeza maudhui ya BBC World Service kwa njia yoyote ile, wala kuchanganya maudhui ya BBC World Service na mambo mengine yoyote.

2.4 Hauruhusiwi kunakili, kusambaza, kupambanua, kubadilisha ufundi, kuchanganu au vinginevyo kukongoroa Wiji ya BBC World Service au kuitumia vifungu vyake kwa njia yoyote ile.

3. Waranti na Shahada


3.1 Wiji ya BBC World Service na Maudhui ya BBC World Service inapatikana kwa utaratibu wa "kama ilivyo" na "kama inavyopatikana" na unapakua, kuisanifisha na kutumia Wiji ya BBC World Service na kutumia Maudhui ya BBC World Service kwa hiari yako na hatari

3.2 BBC imechukua tahadhari ya hali ya juu kuhakikisha Wiji ya BBC World Service na Maudhui ya BBC World Service haina makosa, hitilafu, virusi au upungufu, hata hivyo BBC haitoi hakikisho hilo.

3.3 Kwa kiwango kinachoruhusiwa kisheria, BBC haitoi hakikisho la aina yoyote ( ya kudhaniwa au vinginevyo) kuhusiana na Wiji ya BBC World Service, Maudhui ya BBC World Service au tovuti ya BBC na BBC haitahusika kwa hasara au uharibifu utakaotokana na au kuhusishwa na Wiji ya BBC World Service au Maudhui ya BBC World Service.

3.4 Unashauriwa kuchukua tahadhari zote zinazostahili kulinda kompyuta yako isipate kuambukizwa virusi.

3.5 BBC inaweza kubadilisha au kuhamisha Maudhui ya BBC World Service kwa matakwa yake na inaweza kuzuia matumizi ya Wiji ya BBC World Service endapo utakiuka Kanuni za Utumiaji.

4. Jumla


4.1 Kanuni za Utumiaji zitatafsiriwa kwa mujibu wa sheria za England na kutekelezwa na sheria za mahakama za England pekee.

BBC © 2012 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.