![]() |
||
![]() Fainali ya 2007 Mwaka 2007 ilikuwa mara ya kwanza kufanyika mashindano ya Faidika na BBC. Takriban michanganuo zaidi ya 5,000 iliwasilishwa kutoka Afrika Mashariki na Kati.
Vijana wawili, Francis Wakara Baraka na Geofrey Kibiki, kutoka Tanzania, Arthur Buliva kutoka Kenya na David Ssegawa kutoka Uganda, waliingia kuchuana fainali. Baada ya mchuano mkali wa kukata na shoka, hatimaye majaji Zablon Karingi Muthaka kutoka Kenya, Humphrey Polepole kutoka Tanzania na Halima Abdallah kutoka Uganda wakamchagua David Ssegawa kuwa mshindi. Washiriki watatu waliongia fainali, Francis Baraka na Geofrey Kibiki wa Tanzania na Arthur Buliva wa Kenya walizawadiwa fedha taslimu na simu za mkononi kila mmoja. Fainali hiyo ilirushwa moja kwa moja kupitia BBC Idhaa ya Kiswahili, kutoka Jijini Dar Es Salaam, Tanzania, kwenye mtandao bbcswahili.com na vilevile kupitia kituo maarufu cha televisheni nchini Tanzania ITV na pia EATV kinachorusha matangazo yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Mashindano ya Faidika na BBC yalifanyika kwa mara ya kwanza kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Idhaa ya Kiswahili ya BBC. |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
| ^^ Rejea juu | |||