![]() |
||
![]() Washiriki 2008 Burundi
Mshindi aliyewakilisha Burundi kwenye fainali 2008 ni Ashura Kisesa wakati huo akiwa na umri wa miaka 24. Yeye ni mwanafunzi wa uchumi wa kilimo (agronomia) katika chuo kikuu cha Burundi. Wazo lake lilikuwa kutengeneza vyoo vya umma vya kulipia katika miji. Ashura alishiriki katika shindano la Faidika na BBC mwaka uliotangulia lakini hakufaulu. Aliposhinda kwenye fainali ya kitaifa, alisema: “Sikuamini pale jina langu lilipotangazwa. Nina furaha kubwa sana na ninatumaini kwamba nitashinda kwenye fainali huko Kampala.” Kenya Kenya iliwakilishwa na Witness Omoga mwenye umri wa miaka 22 kutoka Kakamega. Witness alikuwa na nia ya kuwekeza kwenye mtambo wa kutengeneza vitambulisho vya shule. Wakati wa shindano alikuwa akijitolea kumsaidia mjomba wake katika biashara ya uchapishaji picha mjini Kakamega.
Rwanda Mshindi wa Rwanda alikuwa mwanafunzi wa miaka 17 kutoka Kigali, Rangira Aime Frederick. Wazo lake la kuzalisha nishati kwa kutumia kinyesi liliwavutia majaji. Rangira alikuwa mwanafunzi wa sekondari mjini Kigali ambako anajifunza lugha kadhaa: Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili na Kinyarwanda. Rangira naye alisema: “Nimefurahi na nina imani ya kushinda na kunyakua hiyo zawadi.” Tanzania Mshindi wa kitaifa kutoka Tanzania ni mwalimu wa kujitegemea mjini Dar es Salaam, Apolinary Joseph Laksh. Baadhi ya mafunzo anayotoa ni somo la biashara. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 angependa kuchoma makaa kwa kutumia taka kama njia moja ya kuwawezesha watu katika maeneo ya vijijini kutumia vyanzo endelevu na vyenye bei nafuu vya nishati: “Shindano hili lilikuwa kali kwelikweli lakini ninahisi niliwapiku wenzangu kwa sababu ya ukakamavu wangu. Sina wasiwasi wowote na kwa hivyo natumai kufanya vyema huko Kampala.” Uganda Derick Kajukano, mwenye umri wa miaka 23 aliiwakilisha Uganda. Derick ana shahada ya biashara. Lengo lake ni kutengeneza mifuko akitumia taka ya plastiki. Alisema alivutiwa mno na mshindi wa mwaka jana David Ssegawa kutoka nchini humo: “Nilipomsikia akitetea wazo lake hewani, papo hapo nikaanza kujiandaa. Ninafurahi sana kwa kuwa ninakaribia zawadi nono.” Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Hatukuweza kupata washindi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kutokana na kupata michanganuo michache na ambayo haikuweza kufikia viwango muhimu vya mashindano. Mwaka 2009 inatarajiwa Kongo itatoa washindani wakali. |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
| ^^ Rejea juu | |||