|
Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani, UN Habitat, limetoa ripoti inayozungumzia tabaka lililopo katika miji kwa wakazi
wenye kipato kikubwa na wale walio na kipato duni.
Tabaka hilo ni kubwa na linatishia ubora wa miji mbalimbali duniani na hali ya wakazi wake hasa wenye kipato duni.
Ripoti hiyo itakuwa ni ajenda kuu itakayojadiliwa katika Kongamano la tano la mipango miji duniani, litakalofanyika mjini
Rio De Jenairo, Brazil hivi karibuni.
Akizungumza mjini London, mkurugenzi mtendaji wa shirika la makazi duniani, UN Habitat, Profesa Anna Tibaijuka alieleza kuwa
nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zinahitaji kufanya marekebisho makubwa ya sera zao za makazi na kuzitekeleza.
|