Skip to main contentAccess keys helpA-Z index
BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 11 Machi, 2010 - Imetolewa 10:17 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Watu 49 kushitakiwa kwa mauaji Nigeria
 
Polisi nchini Nigeria wanasema watu 49 watashitakiwa kwa mauaji, kufuatia ghasia za kijamii zilizosababisha mamia ya vifo vya watu.

Msemaji wa polisi Mohammed Lerama ameiambia BBC kuwa wengi wa watakaoshitakiwa ni Waisilamu kutoka kabila la Fulani.

Bw Mohammed amesema idadi ya watu waliokamatwa tangu kutokea kwa mauaji hayo katika mji wa Jos imefikia watu 200.

Polisi wanasema watu 109, wengi wao wakidhaniwa kuwa ni Wakristo, walikufa katika mapigano yaliyotokea siku ya Jumapili. Taarifa za awali zilisema idadi ya waliouawa ilikuwa zaidi ya 500.

Ghasia hizo zilifuatia mauaji yaliyochochewa na imani za kidini, karibu na mji wa Jos mwezi Januari, na kusababisha vifo vya watu 300, wengi wao wakiaminika kuwa ni Waisilamu.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha