Skip to main contentAccess keys helpA-Z index
BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 07 Desemba, 2009 - Imetolewa 16:34 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Maonyesho ya picha za ghasia, Kenya
 
Maonyesho ya picha za ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya yameanza kwenye mojawapo wa barabara kuu katika mji mkuu Nairobi.

Picha hizo zinatafsiriwa kama mojawapo ya njia za kuleta maridhiano baina ya jamii mbali mbali ingawaje kumekuwa na pingamizi kutoka kwa polisi na pia baadhi ya raia.

Baadhi ya waliohudhuria maonyesho hayo yalioandaliwa na shirika la Picha Mtaani kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la maendeleo UNDP, ni watu walioathirika na waliotekeleza ghasia hizo.

Baada ya Nairobi, maonyesho hayo pia yatapelekwa katika miji mingine mitano ambayo iliathirika zaidi wakati wa ghasia za uchaguzi mkuu wa 2007/2008.

Zaidi ya watu 1300 walifariki kwenye ghasia hizo huku maelfu ya wengine wakikimbia makaazi yao.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha