|
Askari wa Mugabe waondoka migodini
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Zimbabwe imesema inawaondoa askari wake kwenye migodi ya almasi mashariki mwa nchi hiyo kufuatia mapendekezo yaliyotolewa
na Kimberly Process.
Kimberly Process ni chombo kinachoratibu biashara ya almasi duniani. Mapema mwezi huu, jopo la Kimberly lilitoa miezi sita kwa Zimbabwe kuimarisha mazingira katika eneo linalochimbwa almasi iitwayo Marange. Jopo hilo linaishutumu jeshi la Zimbabwe kwa mauaji na kulazimisha watu kuondoka eneo la migodi hiyo. Waziri wa madini nchini humo Obert Mpofu ameliambia gazeti la serikali la Herald kwamba Zimbabwe imefanya mengi kuhakikisha masharti yaliyowekwa na jopo hilo yanafuatwa. Bw Mpofu pia amesema kulikuwa hakuna tena majeshi ya usalama katika eneo hilo. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||