BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 12 Novemba, 2009 - Imetolewa 03:03 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Obama na mikakati ya Afghanistan
 
Rais wa Marekani Barack Obama amekutana na kamati yake ya usalama wa taifa kujadili mikakati ya Afghanistan, huku tetesi zikiongezeka kuhusu uamuzi wa idadi ya wanajeshi wanaopigana huko.

Maafisa wa Ikulu ya Marekani wamesema rais Obama amejadili suala la muda na mapendekezo manne yaliyowasilishwa na washauri wake, lakini hakuna uamuzi wowote umefikiwa.

Maafisa wa Ikulu wameongeza kuwa rais huyo amesema nia ya Marekani haitomalizika bila dira, na kuwa utawala bora lazima upige hatua.

Waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown ameliambia bunge la nchi hiyo kuwa anatarajia uamuzi kutangazwa hivi karibuni.

'Nimezungumza na Rais Obama na ninatarajia atatangaza uamuzi huo siku chache zijazo, na ni wanajeshi wangapi watahusika,' Bw Brown amewaambia wabunge.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha