BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 11 Novemba, 2009 - Imetolewa 12:15 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Maafa zaidi Afrika kutokana na saratani
 
Vifo kutokana na saratani vitaongezeka barani Afrika, ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo.

Kulingana na wanasayansi wa Marekani, ongezeko hilo ni kutokana na sheria chache barani Afrika kuzuia uvutaji sigari wa kiholela.

Wanaovuta sigara wataongezeka maradufu katika kipindi cha miaka 12 ijayo, ikiwa mwenendo huu hautapunguza kasi, kulingana na shirika linalohusika na saratani nchini Marekani (American Cancer Society).

Ripoti ya shirika hilo inaelezea kwamba zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaoishi barani Afrika hawana kinga yoyote kutokana na moshi unaotoka kwa wavutaji sigara.

Baadhi ya mataifa ya Afrika yana sheria za kuzuia uvutaji sigara hadharani, lakini mataifa mengi bado hayana vikwazo vyovyote.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha