|
Alex Wiens alikaa nyuma ya glasi isiyopitwa na risasi akizungukwa na wanausalama wakati wa hukumu ya maisha. Itakumbukwa kua
ni mwezi julayi, alipompiga kisu na kumuua Marwa el Sherbini katika mahakama hio hio.
Ujeremani ni nchi ya pili kwa kua na idadi kubwa ya Waislamu barani Ulaya na tukio hilo lilizua ghadhabu katika mataifa ya
Waislamu baada ya Ujerumani kuchelewa kulaani kisa hicho.
Mamiya ya Waislamu walikusanyika nje na kusali wakiitaka serikali iwajibike zaidi dhidi ya ubaguzi. Wakati wote huo Alex Wiens
ambaye ni raia wa Ujerumani, mzaliwa wa Urussi alidai kua hakukusudia. Lakini mwanasheria mkuu wa Ujerumani alisema ni bayana
kwamba sababu yake kuu ni chuki kwa waislamu.
|