|
Mauaji ya mtoto yaibua hasira A.Kusini
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Mkuu wa polisi wa Afrika Kusini amelaani ufyatuliaji risasi kwa mtoto wa kiume wa umri wa miaka mitatu yaliyofanywa na ofisa
wa polisi.
Bheki Cele ameyapuuza madai ya afisa huyo kwamba alifyatua risasi kujihami akiamini bomba alilokuwa ameshika mtoto huyo ni bunduki. Ameiambia BBC kwamba mauaji hayo ni uhalifu wa kizembe akisema: "Hata kama ingekuwa bunduki ya kweli, usingeanza kufyatua risasi." Lakini alitetea haki ya polisi kuweza kutumia nguvu inapobidi. Atlegang Aphane alikuwa ndani ya gari ambalo polisi walidhani linaendeshwa na wanaoshukiwa kuwa wahalifu alipopigwa risasi
siku ya Jumanne. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||