BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 10 Novemba, 2009 - Imetolewa 02:38 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Rufaa kumnusuru mdunguaji Marekani nje
 
Mahakama Kuu ya Marekani imekataa rufaa ya mawakili wa mdunguaji aliyeuwa watu mwaka 2002 mjini Washington DC waliotaka kucheleweshwa hukumu hiyo.

John Allen Muhammad anatazamiwa kunyongwa leo Jumanne kwa kumuua Dean Harold Meyers, mmoja wa watu 10 waliouawa wakati wa wiki tatu za mashambulio.

Mahakama hiyo haikutoa sababu ya kukataa maombi hayo ya kumhurumia.

Muhammed bado anayo nafasi moja ya mwisho ya kupewa msamaha na Gavana wa Virginia, Timothy Kaine.

Mtoto wa Muhammad wakati huo akiwa mvulana, Lee Boyd Malvo, anatumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela kutokana na kushiriki katika mauaji hayo.

Watu hao wawili waliwauwa watu sita mjini Alabama na Louisiana kabla ya kuhamia Maryland, Washington na Virginia.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha