BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 10 Novemba, 2009 - Imetolewa 02:21 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Miaka 20 ya ukuta wa Berlin sasa vitendo
 
Igizo wakati wa kuadhimisha miaka 20 ya kuangushwa ukuta wa Berlin
Maadhimisho ya miaka 20 ya kuangushwa ukuta wa Berlin yafana
Viongozi waliohudhuria maadhimisho ya miaka 20 tangu ulipoangushwa ukuta wa Berlin, wamesema harakati dhidi ya madhila sehemu mbalimbali duniani hazina budi kuendelezwa.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wakati wa maadhimisho hayo kwenye lango la Brandenburg alijumuika na Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Waziri wa Mammbo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton.

Viongozi hao wameonya mamilioni ya watu duniani bado wanaedelea wanavunjiwa haki zao za kibinadamu.

Ukuta wa Berlin uliangushwa mwaka 1989 hali iliyosababisha Ujerumani kuungana upya na ndio chanzo cha kuanguka kwa Muungano wa nchi za Urusi na kumaliza vita baridi.

Ujerumani Mashariki iliyokuwa ya Kikomunisti ilijenga ukuta huo wa kilometa 155 mwaka 1961 ikijitenga na Berlin Magharibi hali iliyowazuia raia wake kutorokea magharibi kukimbia siasa za Kikomunisti.

Bi Merkel aliyekulia Ujerumani Mashariki, katika sherehe hizo aliongoza maandamano yaliyopita lango la Brandenburg lililo ishara ya kuunganika upya kwa Ujerumani mwaka 1990.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha