BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 09 Novemba, 2009 - Imetolewa 18:18 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Mradi wa usafiri Afrika Kusini njia panda
 
Moja ya mradi mkubwa wa miundombinu nchini Afrika Kusini, wa matayarisho ya Kombe la Dunia, mwaka ujao, hautakuwa tayari ifikapo wakati huo.

Msemaji wa shirika la reli iendayo kwa kasi - Gautrain - ameiambia BBC kuwa reli hiyo haitaanza kazi rasmi, hadi wiki mbili baada ya michuano hiyo kuanza.

Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg, Jonah Fisher amesema taarifa hizi ni pigo kwa matarajio ya Afrika Kusini kuandaa michuano yenye mafanikio makubwa.

Katika tukio lingine, waandalizi wa Kombe la dunia wamelaani kupaa kwa kodi za nyumba kwa ajili ya tukio hilo.

Mkuu wa kamati ya maandalizi Danny Jordaan amesema bei kubwa zinaweza kuathiri matarajio ya Afrika Kusini ya kuwashawishi watalii kurejea tena baada ya Kombe la Dunia.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha