|
Mwenyeketi katika kashfa ya ubaguzi
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Mwenyekiti wa shirika la umeme nchini Afrika Kusini, Eskom, amejiuzulu baada ya kushutumiwa kwa madai ya ubaguzi wa rangi.
Mwenyekiti huyo Bobby Godsell, ambaye ni mzungu na Jacob Maroga, mwafrika mweusi, walikuwa katika mvutano wa madaraka kwa muda mrefu. Wiki iliyopita Bw. Maroga alijiuzulu, na kusababisha tawi la vijana la chama cha ANC kudai kwamba alisukumwa kando kutokana na rangi yake. Eskom imekuwa ikigonga vichwa vya habari tangu mwaka jana wakati ukosefu wa umeme ulipoikumba nchi hiyo. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||