BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 09 Novemba, 2009 - Imetolewa 17:29 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Meli ya mafuta yanusurika kutekwa
 
Jeshi la kupambana na maharamia la Umoja wa Ulaya limesema maharamia wa kisomali wameshambulia meli ya mafuta, karibu kilomita elfu 2 kutoka pwani ya Somalia.

Meli hiyo iliyosajiliwa Hong Kong, iliweza kukimbia shambulio hilo lililofanywa na vyombo viwili vya majini, vinendavyo kwa kasi. maharamia katika chombo hicho walikuwa wakifyatua risasi na mabomu ya roketi.

Shambulio hili limeelezwa kuwa kuwa la kwanza kufanyika mbali zaidi na pwani ya Somalia.

Wakati huohuo, taarifa za wataalam wa baharini zinasema maharamia wameteka meli ambayo ina shehena ya silaha.

Takriban meli 40 kutoka Umoja wa Ulaya, Marekani, China, India na Japan, zinahusika na shughuli za kupambana na uzuiaji wa utekaji nyara unaofanywa na maharamia, hasa katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha