|
Twiga waongezeka Niger
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Wahifadhi wanyama wa pori nchini Niger wameelezea kuongezeka kwa idadi ya twiga nchini humo, licha ya wasiwasi miaka kumi
iliyopita kwamba wangeliweza kutoweka kabisa.
Wanaelezea kwamba huku idadi yao ikiongezeka, wamekuwa wakihamia hadi makazi mapya. Juhudi katika kuwahifadhi wanyama hao, hasa kutokana na kuungwa mkono na serikali, zimesaidia katika kuongeza idadi ya twiga kutoka 50 hadi karibu 200. Wengi wanapatikana karibu na mji mkuu wa Niamey. Hawa ni aina fulani ya twiga, na ambao awali walipatikana kuanzia Chad adi pwani ya bahari ya Atlantic nchini Senegal. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||