BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 08 Novemba, 2009 - Imetolewa 13:09 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Eritrea yanyanyasa raia wake
 
Ripoti inayoeleza hali ya wafungwa nchini Eritrea, imechapishwa na kituo cha amani na haki za binadam cha mjini Oslo.

Kwa mujibu wa Ripoti hiyo kuna magereza kadhaa, mengine katika visiwa vya mbali katika Bahari ya Sham vijulikanavyo kama Dahlak huku wengine wakiwa ndani ya ma-container.

Wafungwa huning'inizwa juu chini, na kuachwa siku kadha, kwenye jua na mvua na wengine wanapotea tu na miili huonekana mabara-barani.

Mtu yeyote anaweza kukamatwa Eritrea kwa sababu yoyote au bila ya sababu. Na kutokuwepo kwa vyombo huru vya habari, vyama vya upinzani au waandishi wa habari wa kigeni hali inaendelea bila ya kuripotiwa.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha