BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 07 Novemba, 2009 - Imetolewa 13:44 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Mahasimu nchini Madagascar waafikiana
 
mahasimu waafikiana
Andry Rajoelina
Viongozi mahasimu wa kisiasa wa Madagascar wamekubaliana kuunda serikali ya pamoja baada ya mivutano ya miezi kadha.

Kiongozi wa sasa wa Madagascar Andry Rajoelina amesema viongozi wanne wamekubaliana katika mazungumzo yaliyofanyika Addis Ababa, Ethiopia, yeye aendelee kuwa Rais hadi uchaguzi ujao mwakani.

Amesema badala ya kuwa na makamu wa rais, kutakuwa na marais wawili watakaoshirikiana wakiwakilisha vyama vya siasa.

Bw Rajoelina alimpindua Marc Ravalomanana mwezi wa Machi, lakini ameshindwa kutambuliwa na jumuia ya kimataifa.

Bw Rajoelina pamoja na washirikia wake ambao walimshutumu Ravalomanana kwa ufujaji wa fedha za umma, wenyewe wameshutumiwa na Muungano wa Afrika kwa kupindua serikali na misaada kutoka nje ikasimamishwa.

Mahasimu hao wawili pamoja na marais wawili wa zamani, Didier Ratsiraka na Albert Zafy, walikubaliana mwezi wa Agosti kuwa na kipindi cha mpito cha miezi 15, lakini hadi sasa wamekuwa wakivutana juu ya makubaliano hayo.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha