|
ICC kuharakisha kesi watuhumiwa Kenya
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu, amesema ataharakisha kesi za watuhumiwa waliochechea vurugu baada
ya uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka 2007.
Mwendesha mashataka huyo Luis Moreno Ocampo amesema kesi mbili au tatu zitafikishwa mahakamani mwezi wa Julai mwakani. Bw Ocampo amesema "kasi" ni muhimu hali itakayofanya Kenya kuendesha uchaguzi wake mkuu ujao wa mwaka 2012 bila ya vitisho vya kutokea machafuko. Bw Ocampo aliwaambia waandishi wa habari mjini Nairobi wakati akimaliza ziara yake ya siku tatu "Kila mtu ana hofu kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao wa Kenya mwaka 2012. Ndio maana ninaelewe umuhimu wa kuharakisha kesi hizi." Alidokeza kesi hizo huenda zitafanyika Kenya ama Arusha nchini Tanzania ambapo watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 kesi zao zinaendeshwa. Baada ya kukutana mwendesha mashtaka huyo mkuu mwanzoni mwa wiki, serikali ya Kenya ilisema itashirikiana na mahakama ya ICC. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||