|
Jeshi DRC latumia "misaada kama chambo"
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Shirika la misaada la madaktari wasio na mipaka MSF, limedai jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, lilitumia kliniki za
chanjo kama chambo kuwashambulia raia.
Shirika hilo limesema maelfu ya Wahutu walilengwa walipofika katika maeneo ya kliniki zilizoandaliwa kutoa chanjo dhidi ya magonjwa ya surua kwenye maeneo ya waasi. Limelaani mashambulio ya Kivu ya Kaskazini na kuyaita "uovu dhidi ya ubinadamu". Siku ya Jumatatu Umoja wa Mataifa uliacha kuyaunga mkono majeshi ya serikali baada ya kuwashutumu wanajeshi kuuwa raia 62. MSF limesema kliniki hizo zilishambuliwa licha ya kuhakikishiwa ulinzi kutoka pande zote ili kazi ya kutoa chanjo ifanyike katika wilaya ya Maisisi kaskazini magharibi mwa mji wa Goma. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||