BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 06 Novemba, 2009 - Imetolewa 01:20 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
MDC ya Zimbabwe yasitisha mgomo
 
Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amekitaka chama chake kusitisha mgomo dhidi ya serikali ya muungano na rais Robert Mugabe.

Bw Tsvangirai amesema anampa Bw Mugabe siku 30 kutekeleza makubaliano ya kugawana madaraka, hasa kwa mambo muhimu waliojadili.

Waziri mkuu huyo alizungumza hayo baada ya mkutano unaofanyika nchini Msumbiji.

Bw Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change waliigomea serikali Octoba 16.

Marais wanne kutoka kusini mwa Afrika wamekutana kwenye mji mkuu wa Msumbiji, Maputo kusitisha mgomo unaotishia nchi hiyo kuzidi kuingia kwenye mgogoro.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha