|
Saudia yaiondoshea vikwazo Somalia
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Saudi Arabia imeondoa vikwazo vya kuingiza mifugo kutoka Somali vilivyowekwa miaka tisa iliyopita kuzuia kuenea kwa homa ya
Rift Valley.
Baadhi ya wachungaji na wafanyabiashara wamefurahishwa na hatua hiyo. Inamaanisha kuwa wataweza kufaidika kutokana na mifugo hiyo kuhitajika sana wakati wa sikukuu ya Eid al-Adha ambapo waislamu aghlabu huchinja mnyama. Uuzaji wa kondoo, mbuzi na ng'ombe nje ya nchi ni uti wa mgongo wa uchumi wa Somalia na Saudi Arabia ilikuwa soko lake kuu. Nchi ya Somalia iliyopo kwenye pembe ya Afrika haijawa na serikali thabiti tangu mwaka 1991. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||