BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 06 Novemba, 2009 - Imetolewa 05:10 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Vijana wa Nigeria waichapa N.Zealand
 
Timu ya vijana wenye umri ulio chini ya miaka kumi na saba inasherehekea kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia la vijana wenye umri huo nchini Nigeria.

Hii ni baada ya kuifunga New Zealand mabao 5 - 0 mjini Abuja jana jioni.

Hadi mapumziko Nigeria ilihesabu mabao mawili ya Edafe Egbede na moja la Stanley Okoro na baada ya mapumziko Sani Emmanuel akaongezea mawili kuiona Nigeria ikibaki peke kati ya Timu za Afrika katika Kombe hili.

Nigeria sasa itapambana na Korea ya kusini iliyofuzu baada ya kuinyuka Mexico kwaz matuta 5 - 3 baada ya kipindi cha dakika 90 kumalizika pande zote zikihesabu 1-1.

Kabla ya Nigeria kufuzu Burkina Faso ilikuwa tayari imefungishwa virago na Uhispania iliyoichapa 4 -1 mjini Kano.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha