|
Mamluki wanne wa Afrika kusini waliofungwa jela kwa kuhusika na njama ya kupindua serikali ya Equatorial Guinea, hawatakamatwa
tena watakaporejea nchini mwao.
Njama hiyo hata hivyo ilitibuka. Kwa mujibu wa naibu waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini, Ibrahim Ibrahim, watu hao tayari
wameadhibiwa vya kutosha kwa kosa lao.
Watu hao pamoja na mamluki mwigine muingereza, Simon Mann walisamehewa na kiongozi wa Equatorial Guinea wiki jana.
Vitendo vya Mamluki vimepigwa marufuku nchini Afrika kusini lakini mtu hawezi kuhudumia kifungo gerezani mara mbili kwa kosa
moja.
|