BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 06 Novemba, 2009 - Imetolewa 13:56 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
TP huenda wakawa mabingwa Afrika
 
Lomana LuaLua
DRC imewahi kutoa washambulizi wengi wenye sifa kama za LuaLua na bila shaka Mazembe haitakosa wachezaji kama hao
Klabu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ya soka, TP Mazembe, huenda ikawa bingwa wa Afrika kesho Jumamosi, baada ya miaka 41, ikiwa itaishinda Heartland kutoka Nigeria mjini Lubumbashi.

TP Mazembe ilishindwa magoli 2-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza Nigeria.

Hakuna hata mchezaji mmoja wa Congo alikuwa amezaliwa wakati timu ya Congo ya 'Crows', yaani Kunguru, ilipoishinda Etoile Filante ya Togo jumla ya magoli 6-4 na kulihifadhi kombe hilo miaka 41 iliyopita.

Timu hiyo iliyoanzishwa na watawa wa Benedict miaka 70 iliyopita, na ikijulikana kama TP Englebert, iliandikisha historia kwa kuwa timu ya kwanza kufanikiwa kulihifadhi kombe.

Rekodi ilidumu kwa miaka mingi, hadi Enyimba ya Nigeria ilipofanikiwa kulihifadhi kombe hilo mwaka 2004.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha