|
Eneo la maziwa makuu lasaidiwa
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Mkutano wa kimataifa wa waihsani unaofanyika nchini Burundi unatarajia kukusanya zaidi ya dola za kimarekani bilioni moja.
Fedha hizo ni kwa ajili ya kufadhili miradi ya kimaendeleo katika eneo la maziwa makuu barani Afrika. Mmoja wa waandaaji wa mkutano huo, Liberata Mulamula, amesema nchi waihsani wanatakiwa kuhakikisha kuwa eneo hilo lina amani na usalama thabit. Amesema hatua hiyo ni muhimu kuetekelezwa kama ilivyoahidiwa katika mkataba ujulikanao kama Makubaliano ya Nairobi. Makubaliano hayo yalitiwa saini na nchi 11 za Afrika zilizokumbwa na migogoro. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||