|
Ni rasmi sasa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC itawafungulia mashtaka washukiwa wakuu wa machafuko ya baada
ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 nchini Kenya.
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo aliye nchini Kenya Louis Moreno-Ocampo amesema kuwa ataanzisha uchunguzi dhidi ya
washukiwa wakuu wa machafuko hayo mwezi Ujao.
Ocampo ameyasema haya aliopohutubia waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufanya mkutano wa faragha na rais Mwai Kibaki
na waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga mjini Nairobi.
Kwa Upande wake Kenya imesema kuwa itashirikiana na mahakama hiyo ya ICC.Waziri mkuu Raila Odinga amesema kuwa serikali
itafanya hivyo ili kuhakikisha kuwa yale yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 hayatokei tena.
|