BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 05 Novemba, 2009 - Imetolewa 01:31 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Moreno-Ocampo azungumza nchini Kenya
 
Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC, Luis Moreno-Ocampo, anatarajiwa kufanya mazungumzo nchini Kenya siku ya Alhamis.

Mazungumzo hayo ni namna ya kuhakikisha haki inatendeka kwa wale wanoshukiwa kuhusika na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mwaka 2008.

Bw Moreno-Ocampo amesema kama serikali ya Kenya itashindwa kuchukua hatua zozote, basi yeye mwenyewe atashinikiza hatua zichukuliwe.

Zaidi ya watu elfu moja waliuawa katika ghasia hizo.

Uchunguzi wa serikali ya Kenya mapema mwaka huu ulipendekeza suala hilo kupelekwa katika mahakama hiyo ya ICC, the Hague lakini inaweza isfikishwe iwapo mahakama maalum itaundwa nchini humo.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha