BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 05 Novemba, 2009 - Imetolewa 12:54 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Timu za F1 zinapigwa vita - Ferrari
 
Gari la timu ya Ferrari
Timu ya Ferrari ilishindwa kuwika katika mashindano ya msimu 2009
Timu ya Ferrari imetangaza kwamba waliopewa jukumu la kusimamia mashindano ya magari ya Formula 1 wamekuwa wakiyapiga vita makampuni makubwa ya kuunda magari, na timu kadha kulazimika kujiondoa katika mashindano hayo.

Toyota ilitangaza siku ya Jumatano uamuzi wa kujiondoa katika mashindano hayo.

Hayo ni baada ya kuondoka kwa Honda na BMW, huku Renault ikisema bado inafikiria kama itaendelea kuwepo katika mashindano au la.

Taarifa ya Ferrari imeelezea maoni hayo mara tu baada ya mabadiliko katika baraza linalosimamia mashindano ya magari, FIA.

Madaraka ya rais Max Mosley sasa yamechukuliwa na aliyekuwa mkuu wa Ferrari hapo zamani, Jean Todt.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha