|
Wakimbizi wakimbilia Congo-Brazzaville
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Shirika linaloshughulikia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limesema maelfu ya wakimbizi wamevuka mpaka wa Congo-Brazzaville.
Wakimbizi hao wanakimbia ghasia zilizopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Taarifa zinasema polisi 47 wameuawa kufuatia mapigano ya kikabila yalipozuka kwenye jimbo la Equateur huko Jamhuri ya Kongo wiki iliyopita. Wakimbizi wamewaambiwa waandishi kwamba vijiji kadhaa viliunguzwa na watu wengi kuuawa. Serikali ya Congo-Brazzaville imeiomba Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kutoa misaada kwa wakimbizi hao. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||