|
Mpambanaji wa ufisadi auawa Liberia
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Watu wenye silaha nchini Liberia wamemwuua afisa mmoja aliyekuwa akihusika na kupambana na ufisadi hasa katika mikataba ya
umma.
Keith Juba alipigwa risasi mfululizo siku ya Jumapili usiku nje ya nyumba yake, ambapo ni kilomita 60 kutoka mji mkuu wa Monrovia. Hadi sasa polisi hawajasema iwapo mauaji hayo yana uhusiano na nafasi aliyokuwa nayo Bw Jubah ya mkuu wa tume inayoshughulikia mikataba ya umma. Tume hiyo huhakikisha kuwa mikataba hasa ile mikubwa inayohusu migodi ni halali. Mmoja wa ndugu zake Bw Jubah ambaye hakutaka jina lake litajwe ameiambia BBC kuwa mwili wake uliwaka moto. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||