BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa:
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
E Guinea yamsamehe Mann
 
Mwanajeshi wa zamani wa uingereza Simon Mann, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 34 kwa kupanga mapinduzi nchini Equatorial Guinea,amepewa msamaha,serikali imesema.

Mshauri wa rais, Miguel Mifuno,ameiambia BBC kuwa Mann alilazimika kuondoka nchini katika muda wa saa 24.

Wizara ya mambo ya nje ya uingereza imesema inafahamu kuwa kuachiliwa huru kwa Mann ni uamuzi binafsi wa rais kwa misingi ya kibinadamu.

Mann, aliyehukumiwa kifungo mwezi Julai mwaka 2008, alikiri kula njama ya kumpindua rais Teodoro Obiang Nguema wakati wa kesi yake.

Bwana Mifuno amesema Mann aliachiliwa huru kwa misingi ya kibinadamu kuhusiana na afya yake.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha