BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 03 Novemba, 2009 - Imetolewa 11:45 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Congo yakerwa na UN kuinyima msaada
 
Umoja wa mataifa, umekemewa na serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa kusitisha msaada kwa wanajeshi wa serikali wanaopambana dhidi ya makundi ya waasi.

Waziri wa habari na mawasiliano Lambert Mende amefahamisha BBC kwamba hana ufahamu wowote kuhusu mauaji yanayodaiwa na umoja huo kutekelezwa na jeshi la serikali.

Hiyo ndio sababu imepelekea umoja huo kusitisha msaada kwa jeshi la serikali.

Umoja wa mataifa umedai kuwa watu sitini na wawili waliuawa na jeshi la Congo huku mashirika ya kijamii yakituhumu jeshi hilo kwa kuwabaka na kuwaua wanawake.

Waasi hao wa kihutu walitoroka Rwanda mwaka 1994 baada ya kushutumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha