BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 02 Novemba, 2009 - Imetolewa 12:51 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
UN yajitenga na jeshi la Congo
 
Umoja wa mataifa umesitisha kuunga mkono kitengo cha jeshi la jamhuri ya kidemokrasi ya Congo,ikishutumu wanajeshi kwa mauaji ya watu 62,afisa mmoja mkuu wa umoja wa mataifa amesema.

Mkuu wa vikosi vya kulinda amani wa umoja wa mataifa Alain Le Roy amesema kuwa ana taarifa kwamba jeshi ''lililenga kwa maksudi'' raia.

Watetezi wa haki za binaadamu wamesisitiza kuwa watu wa kabila la wahutu wamekuwa wakiuawa na wanajeshi wa Congo, na wamelaumu umoja wa mataifa kwa kutojitahidi kuzuia mauaji hayo.

Umoja wa mataifa umekuwa ukisaidia jeshi kukabiliana na waasi wa kihutu wa Rwanda tangu mwezi Januari.

Kufwatia ziara ya eneo hilo, bwana Le Roy alisema jeshi limewaua raia 62 kati ya mwezi mei na septemba mwaka huu.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha