|
Kimunya ajiuzulu uwaziri Kenya
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Waziri wa Fedha wa Kenya Bw Amos Kimunya anaachia ngazi huku uchunguzi ukiendelea kuhusu utata unaozingira hatua ya kuuzwa kwa hoteli moja ya kifahari katika mji mkuu Nairobi. Bw Kimunya alieleza kwamba amemwomba rais Mwai Kibaki amruhusu kujiuzulu kuwezesha uchunguzi kufanyika.Msemaji wa serikali amefahamisha kwamba hatua hiyo ya kujiuzulu ni ya muda mfupi. Mpasuko Utata unaotanda kuuzwa kwa hoteli ya Grand Regency umesababisha mpasuko katika serikali ya umoja iliyoundwa kumaliza ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Bw Kimunya ambaye ni swahiba wa rais Kibaki, amekanusha taarifa kwamba hoteli hiyo iliuzwa kwa kampuni moja ya Kenya yenye uhusiano na Libya kwa gharama ambayo ni theluthi ya thamani yake halisi. "Kama nilivyokwisha eleza kabla, dhamira yangu ni wazi kabisa, na msimamo wangu ni ule ule kwamba niko wazi kwa uchunguzi huria kufanyika kuhusu kuuzwa kwa Grand Regency Hotel," Bw Kimunya alieleza katika mkutano na waandishi wa habari. Waziri huyo wa fedha amekuwa katika majadiliano na rais kuhusu swala hili," alieleza msemaji wa serikali Alfred Mutua, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters. "Lakini nafasi yake haitajazwa na mtu mwingine, ni hatua ya muda tu." Uchunguzi uliofanywa na mwanasheria wa serikali juma lililopita ulihitimisha kwamba Bw Kimunya anatakiwa kusimamishwa kazi. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||