Imeandikwa na BBC London.
|
 |
 |
|
| Nchi wahisani zinajaribu zaidi kutumia diplomasia kutuliza ghasia badala ya vikwazo. |
Pande zote mbili katika mzozo wa uchaguzi wa Kenya zimetupiana lawama za kuchochea ghasia huku jitihada za kidiplomasia zikifanyika
kutuliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Watu wasiopungua 275 wameuawa, wakiwemo 30 magharibi mwa Kenya ambao walichomwa moto ndani ya kanisa walikoenda kuomba hifadhi.
Idadi kubwa ya wananchi wamekuwa wakiomba hifadhi katika maeneo salama kuepuka magenge ya watu wenye silaha na waporaji mali
huku wasi wasi ukizidi wa mashambulio zaidi na kulipizana visasi.
Polisi katika mji mkuu Nairobi wameweka vizuizi vya barabarani kwenye maeneo muhimu ya kuingilia katikati ya jiji na kudhibiti
mwenendo wa magari.
Pamoja na hali kuonekana kuanza kuwa tulivu, bado kuna wasi wasi kwamba ghasia zinaweza kuzuka upya endapo mkutano wa wapinzani
ulioitishwa kesho utafanyika.
|