http://www.bbcswahili.com

21 Septemba, 2009 - Imetolewa 22:34 GMT

Imeandikwa na Peter Musembi

Zuma akiri kutokubaliana na wafanyakazi

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema suala la kutoafikiana linadumu baina ya chama tawala cha ANC na Shirikisho la wafanyakazi (Cosatu) moja ya mshirika wake mkubwa kisiasa.

Chama cha ANC hivi karibuni iliikasirisha Shirikisho la Wafanyakazi baada ya kupinga kuwepo shirikisho hilo jeshini na Bwana Zuma akazidi kukazia suala hilo katika hutuba yake alipozungumza katika mkutano mkuu wa Cosatu.

Lakini hata hivyo Rais Zuma alisisitiza kuwepu umoja na kusema chama cha ANC ni sawa na ''kanisa kubwa'' linaloweza kuafiki bila ya kusutwa.

Bwana Zuma alitegemea kwa kiasi kikubwa msaada wa Shirikisho la wafanyakazi limuunge mkono alipochaguliwa kuwa rais katika uchaguzi mkuu mapema mwaka huu.

Na Cosatu inaaminika ndyo shirikisho kubwa zaidi kati ya mashirikisho matatu ya wafanyakazi ya kitaifa nchini Afrika Kusini.

Bwana Zuma ameitisha mkutano mkubwa ili wazungumze namna ya kuondoa tofauti zao.