|
Pembe haramu zanaswa nchini Kenya
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Maafisa wa huduma za wanyama wa pori nchini Kenya, KWS, wamenasa pembe za ndovu na vifaru weusi zikiwa zimefichwa katika jeneza
lililokuwa likisafirishwa kwa ndege hadi Laos.
Thamani ya pembe hizo 16 inakadiriwa kuwa dola za Marekani milioni moja. Kwa mujibu wa maafisa hao, damu iliyopatikana kwa pembe hizo zenye uzani wa kilogramu 300 zilinyofolewa kutoka kwa tembo na vifaru hivi majuzi. Ndege hiyo ilikuwa imetoka Msumbiji na kutua mjini Nairobi ikiwa safarini kuelekea nchini Thailand na hatimaye Laos. Asili ya pembe hizo haijulikani ingawa maafisa wa KWS wanasema kwamba huenda zilitolewa nchini Tanzania au Afrika Kusini. Kifaru mweusi ni mnyama adimu sana na hupatikana tu katika maeneo ya mashariki na kusini mwa Afrika. Biashara ya pembe za ndovu na wanyama kama vile kifaru mweusi ambao idadi yao inaendelea kudidimia, ilipigwa marufuku mnamo mwaka wa 1989. Lakini baadhi ya nchi hazitekelezi marufuku hiyo. |
VIUNGO VYA MTANDAO WA HAPA HAPA
Profesa Haroub Othman azikwa Zanzibar29 Juni, 2009 | Habari
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||