BBC navigation

'Kimbunga' cha mabao chapiga Brazil

Imebadilishwa: 9 Julai, 2014 - Saa 13:41 GMT

Kimbunga Brazil

 • Bao la kwanza la Ujerumani lilipokewa kwa vifijo na nderemo na mashabiki waliokuwa wamejaa pomoni kushuhudia timu yao ikimenyena na mabingwa mara sita wa kombe la dunia Brazil
 • Mechi hii ilikua ya kwanza ya nusu fainali katika kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil
 • Wengi wamesema wachezaji wa Ujerumani walikuwa 'balaa' yaani walikuwa wakali katika mechi hiyo
 • Kipa wa Ujerumani hakuwa na chochote cha kufanya kwani hali ilikuwa ngumu kweli.
 • Ilikuwa sherehe kila pembe ya dunia kutoka kwa mashabiki wa Ujerumani na hata nyumbani baada ya timu yao kuingiza mabao matano katika dakika za kwanza 29 za mechi hiyo
 • Mabao yaliendelea kuingizwa hadi yakafika saba mwishoni mwa mechi. Brazil hata hivyo walikomboa bao moja la kupanguzia machozi, ila halikutosha kuondoa aibu waliyoipata katika mchuano huu ambao umewaacha wengi vinywa wazi
 • Mashabiki wa Brazil walikuwa wanajionea giza uwanjani magoli yakiingizwa na Ujerumai kutoka pembe zote za uwanja
 • Ujerumani sasa watajiandaa kumenyana na mshindi wa mechi kati ya Uholanzi na Argentina Brazil itasalia kupigania nafasi ya tatu
 • Huzuni ulitanda Brazil na kote duniani kwa mashabiki wa Brazil
 • Lakini nahodha wa muda wa Brazil David Luiz amewataka mashabiki wa timu hiyo kote duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa uwanjani Selecao,walipoadhibiwa kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
 • Kwa sasa hadi fainali za kombe la dunia ni sherehe kote kote nchini Ujerumani

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.