Arsenal yazoa alama tatu dhidi ya Stoke

  • 2 Februari 2013
Mchezaji wa Arsenal

Mchezaji wa ziada Lukas Podolski, aliifungia Arsenal bao moja na kuipa alama tatu muhimu, katika kinyang'anyiro cha kuwania kombe la ligi kuu ya Premier ya England.

Bao hio la pekee lilifufua matumaini ya Arsenal dhidi ya Stoke City katika mechi kali iliyochezwa katika uwanja wa Emirates.

Kipa wa Stoke City Asmir Begovic aliokoa makombora ya mshambulizi wa Arsenal Lukas Podolski, kunako dakika za mwisho za mechi hiyo.

Begovic vile vile alizuia mikwaju ya Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye alikuwa amesalia pekee ndani ya eneo la hatari.

Katika mechi zingine, QPR ilitoka sare ya kutofungana baop lolote na Norwich City.

Everton vile vile ilitoka sare ya kufungana magoli matatu kwa matatu na Aston Villa.

Reading imejizolea alama tatu zaidi baada ya kuinyuka Sunderland Magoli mawili kwa moja, Swansea ikaambulia patupu ugenini kwa kulazwa moja bila na West Ham.

Wigan licha ya kuwa katika uwanja wao wa nyumbani ililazimika kugawana alama na Southampton baada ya kufungana magoli mawili kwa mawili.