bbc.co.uk navigation

Chisora amzaba kofi Klitschko

Imebadilishwa: 17 Februari, 2012 - Saa 19:11 GMT
Dereck Chisora

Klitschko amesema atalipiza kisasi ulingoni kwa kuzabwa kofi na Chisora

Mwanandondi Muingereza ambaye ni mzaliwa wa Zimbabwe, Dereck Chisora amemzaba kofi mpinzani wake Vitali Klistchko kabla ya pambano lao la mjini Munich, Ujerumani, siku ya Jumamosi.

Ripoti zasema Chisora alimrushia kofi Klitschko, ambaye ni bingwa mtetezi wa masumbwi ya uzani wa juu wa tawi la WBC, wakati wa kikao na waandishi wa habari baada ya wote wawili kupimwa uzani wao, tayari kwa pambano la mjini Munich, Ujerumani. Klitschko, ambaye ni raia wa Ukraine, alijizuia kujibu kofi hilo na kukitaja kitendo cha Chisora kama cha kustajabisha.

Chisora, mwenye umri wa miaka 28, amesema licha ya kukosa ujuzi, atampokonya Klitschko taji lake.

Kwa upande wake, Klitschko amejigamba kwamba hakuna upinzani wa kumbabaisha katika harakati za kutetea ubingwa wake.

BBC © 2012 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.