bbc.co.uk navigation

Beckham ataka unahodha

Imebadilishwa: 20 Januari, 2012 - Saa 12:43 GMT
David Beckham

Anatumaini atakuwa nahodha wa timu ya Uingereza ya soka katika Olimpiki

David Beckham ameelezea dhamira yake ya kutaka kuiongoza timu ya Uingereza itakayoshiriki katika michuano ya soka katika mashindano ya Olimpiki mwaka huu wa 2012.

Beckham alitia saini mkataba mpya na timu ya Marekani ya LA Galaxy mapema wiki hii, na kati ya makubaliano aliyoyafanya ni klabu kumruhusu kushiriki katika mashindano ya London.

"Ningelipenda sana kuwa nahodha", mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alielezea. "Nimewahi kuiongoza nchi yangu, na ninaelewa hili ni jambo muhimu sana katika kuiongoza timu katika Olimpiki."

"Nimezungumza na Stuart Pearce (kocha), lakini bado sijachaguliwa."

Beckham alikuwa ni kati ya watu waliokuwemo katika kundi la kuongoza kampeni za London za kuandaa mashindano waliofika Singapore mwaka 2005.

Yeye ni kati ya wachezaji 184 ambao wameandikiwa barua na chama cha soka cha FA nchini England kuthibitisha kwamba wataweza kuichezea timu ya Olimpiki.

"Ningelipenda kuwa kati ya wale watakaoshiriki katika timu ya GB", alielezea, huku akimshukuru Tim Leiweke, rais wa LA Galaxy, wamiliki AEG, na kocha wa Galaxy Bruce Arena, kwa kumruhusu kuondoka MLS kwa muda.

BBC © 2012 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.