Mlemavu Tanzania ajitegemea

14 Agosti 2014 Imebadilishwa mwisho saa 13:54 GMT

Katika jamii mbali mbali Afrika mashariki kumekua na imani kuwa walemavu hawana uwezo wa kujitegemea na kusaidia kuingizia kipato familia zao hivyo walemavu hupita wakiombaomba kwa ajili ya kuweza kujikimu kwa siku

Lakini hali si hivyo kwa baadhi ya walemavu ambao wamekua wakiamini kuwa pamoja na kukumbwa na changamoto ya ulemavu wataweza kujitegemea na kutegemewa na familia zao.

Philip Paul, mlemavu asiyeona ni mkazi wa Tabora, magharibi mwa Tanzania ni mmoja kati ya walemavu ambao haungi mkono tabia za kuranda mitaani na maeneo ya barabarani kuomba kwa wapita njia.

Pamoja na kutoona Philip anafanya biashara ya machungwa na cha kustaajabisha anazitambua sarafu zinazotumika kununua machungwa kwa kuzipapasa.