Je Ilikuwa ajali au ndege ilidunguliwa?

22 Julai 2014 Imebadilishwa mwisho saa 14:00 GMT

Wachunguzi waruhusiwa kuingia eneo la mkasa wa ndege ya Malaysia kubaini chanzo cha kuanguka kwa ndege ya Malaysia
Maafisa nchini Ukraine wanasema kuwa ndege ya abiria iliyoanguka nchini humo ilidunguliwa katika eneo la mashariki mwa taifa hilo ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi vya serikali.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 298 ikiwemo watoto wadogo watatu. Ilikuwa safarini kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur
Mabaki ya ndege ilitapakaa kila sehemu katika ajali hiyo iliyotokea Alhamisi usiku
Haya ni baadhi ya masalia ya ndege hiyo ya muundo wa jet karibu na kijiji cha Grabovo, kinachodhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine
Ndege hiyo nambari MH17 ilikua inakaribia kuingia anga ya Urusi mawasiliano yalipokatizwa.
Rais wa Ukraine Petrop Poroshenko alielezea tukio hilo kuwa ni tendo la kigaidi huku waasi wakikanusha kuidungua. .
Inaaminiwa waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine walizidungua ndege mbili za jeshi la Ukraine katika eneo hilo hivi karibuni.