Vijana wa Kisomali na mitindo yao

24 Machi 2014 Imebadilishwa mwisho saa 20:17 GMT

Vijana wa Kisomali mjini Nairobi wamejitosa katika fasheni na sasa wanalenga kuwa waigizaji
Hii ni mara ya kwanza kwa maonyesho ya mitindo ya kisomali kuandaliwa na kushirikishwa wasomali peke yao. Maonyesho yaliandaliwa mwishoni mwa wiki ambapo vijana kwa wasichana walijitokeza kuonyesha urembo wao na mavazi.
Hawa ni baadhi ya wasichana wanaoenzi mitindo ya aina aina na ambao walishiriki maonyesho hayo yaliyoandaliwa mtaani Eastleigh, viungani mwa Nairobi
Waandalizi wa maonyesho haya walikuwa vijana wanaopenda sanaa mambo ya mitindo na ambao wanataka kujenga himaya ya usanii mtaani Easteligh. Sio mitindo na mavazi tu bali pia wanapigia debe jamii ya wasomali kuwa na filamu zao
Kwa kawaida msichana wa kisomali huwa ni mwenye kujisitiri kikamilifu , aliyefunika nywele zake na kuficha umbo , lakini maonyesho hayo yamewapa fursa wasichana wa kisomali mtaani Easteligh kuonyesha na kujibunia mavazi yao
Hawakuonyesha tu mavazi yanayoonyesha umbo zao bali pia walikwea jukwaani na kuonyesha mavazi ya kujisitiri kwa msichana wa kisomali
Eastleigh ni mtaa wa kisomali ambao wakazi wake wengi ni wasomali waliozaliwa Kenya au waliohama kutoka Somalia. Waandalizi wa maonyesho haya wanasema wanataka Easteligh iwe ngome ya filamu za kisomali na kupewa jina Eastleighwood
Nywele, mapambo ,manukato, mavazi yote yalidhihirika kwenye maonyesho hayo yaliyoandaliwa na wasomali wa Easteligh.
Sio wasichana tu walioshiriki bali pia vijana walijitosa jukwaani kuonyesha urembo wao