Afrika wiki hii kwa picha

23 Machi 2014 Imebadilishwa mwisho saa 19:59 GMT

Udi watumiwa kutengeza manukato Somalia na picha nyinginezo kutoka Afrika
Wachezesha vikaragosi waliendesha kikaragosi hiki wakati wa maonyesho katika barabara za Cape Town Afrika Kusini.
Maonyesho haya yamefikisha mwaka wake wa tano mwaka huu. Maonyesho yenyewe hudumu kwa saa mbili na huanza punde baada ya jua kuchomoza.
Katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, waandamanaji, wanateketeza bendera ya Ufaransa siku ya Ijumaa tarehe 14 kufuatia mauaji ya waisilamu katika nchi jirani ya CAR. Wanajeshi 7,000 wamekuwa wakishika doria,kurejesha usalama nchini humo.
Mkulima katika shamba lake mjini Moulay, Morocco akivuna matunda yajulikanayo kama Forosadi, ambayo yatauzwa nje ya nchi.
Siku ya Ijumaa kulikuwa na maonyesho ya bidhaa mbali mbali kutoka nchini Somalia yaliyofanyika Dubai. Hapa msichana huyu anaonyesha mafuta ya kujipaka na ya kujifukiza yaliyotengezwa kutoka kwa udi.
Watoto wa Madrasa mjini Dakar Senegal ambao wanaamrishwa kwenda katika mitaa ya mji mkuu kuomba omba
Maandamano ya wafanyakazi nchini Afrika Kusini wakilalamikia kile walichosema ni ukosefu wa ajira kwa vijana. Vyama vya wafanyakazi vinasema kuwa nusu ya vijana wa Afrika Kusini wenye umri wa kati ya miaka 15-24 hawana ajira.
Mwanamke huyu alikuwa anaandamana nchini Msumbiji dhidi ya sheria ya kikoloni inayowaruhusu wabakaji kuachiliwa ikiwa watakubali kumuona mtu waliyembaka