Lupita:Kila ndoto hutimia

12 Machi 2014 Imebadilishwa mwisho saa 08:07 GMT

Lupita Nyong'o amekuwa muigizaji wa kwanza mkenya kushinda tuzo ya Oscar katika filamu 12 Years a Slave
Oscars za mwaka huu ziliongozwa na Ellen DeGeneres, ambaye alianza kwa mbwembwe zake huku akijipiga picha kwa simu yake maarufu kama 'Selfie'
Lupita Nyong'o: Nyota wa filamu '12 Years a Slave' alikuwa muigizaji msaidizi na baada ya kuteuliwa kwa tuzo hiyo, alifanikiwa kuinyakua katika hafla ya tuzo za Oscars
Muigizaji msaidizi katika Filamu ya 12 Years, Lupita Nyong'o akionyesha wazi hisia zake baada ya kushinda tuzo hiyo kwa muigizaji msaidizi bora zaidi. Alicheza kama msichana mtumwa ambaye alipendwa na bwenyenye wake
Lupita alimshukuru sana mtengezaji wa filamu hiyo Mwafrika mzaliwa wa Uingereza Steve McQueen na waigizaji wenzake, Chiwetel Ejiofor na Michael Fassbender. Lupita alisema amejifunza mengi sana katika filamu hiyo.
Mtengeza filamu ya '12 Years a Slave' Steve McQueen, aliruka kwa furaha baada ya filamu hiyo kuibuka filamu bora zaidi kwa zote mwaka 2013. Alikumbatiana na Brad Pitt, mmoja wa waliotengeza filamu yenyewe huku McQueen kisema kuwa bila Brad filamu hiyo isingetengezwa.
Cate Blanchett alishinda tuzo ya muigizaji bora zaidi kwa filamu Blue Jasmin
Jioni yenyewe ya Oscars ilijaa waagizaji mashuhuri ambao walikuwa watangazaji kwa siku hiyo, wakiwemo, Jamie Foxx na Jessica Biel, Joseph Gordon-Levitt na Emma Watson na Penelope Cruz pamoja na Robert De Niro.
Kakake Lupita Junior,(kulia) hakutaka kukosa nafasi ya kuonekana miongoni mwa waigizaji mashuhuri na wana Hollywood wakimeo, Meryl Streep, Brad Pit na wengineo
Kristen Bell akihudhuria hafla ya tuzo za Oscars
Alfonso Cuaron akipokea tuzo yake kwa kutengeza filamu ya Gravity. Alikabidhiwa tuzo hiyo na Angelina Jolie