BBC navigation

Ghasia sasa basi Ukraine

Imebadilishwa: 24 Februari, 2014 - Saa 10:14 GMT

Ukraine makabiliano

  • Polisi katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev, wameanza makabiliano mapya dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikali huku idadi ya waliofariki ikifika watu 25
  • Juhudi mpya za kuwaondoa wapinzani katika majengo ya serikali zinakuja wakati Rais Yanukovych akilaumu viongozi wa upinzani kwa kusababisha ghasia mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo.
  • Baada ya mazungumzo yaliyofanyika usiku kucha kugonga mwamba, aliwasihi kujitenga na makundi yenye siasa kali
  • Wanaharakati wanasema kuwa ghasia zimechochewa na maafisa wakuu wa upinzani
  • Polisi wamedhibiti sehemu moja ya mji kwa mara ya kwanza tangu mwezi Disemba
  • Polisi wameanzisha harakati zao dhidi ya wafuasi wa upinzani katika medani inayojulikana kama Maidan hii leo. Kambi za waaandamanaji hao ziliteketezwa na polisi wakatumia maji kuwatawanya.
  • Katika taarifa kwa vyombo vya habari, wizara ya afya ilisema kuwa idadi ya waliofariki imefika 25. Tisa kati ya waliouawa ni polisi.
  • Mamia ya watu wamepokea matibabu na kuna hofu kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka zaidi
  • Maandamano yalinza mwezi Novemba wakati ambapo Rais Victor Yanukovych alipokataa kujiunga na Muungano wa Ulaya kwa maswala ya kiuchumi
  • Ghasia zilizuka nje ya bunge siku ya Jumanne asubuhi wakati wafuasi wa serikali walipojitokeza kukabiliana na waandamanaji wa upinzani katika juhudi za kutaka kupunguza mamlaka ya kikatiba ya Rais wa nchi hiyo

Shutuma kutoka jamii ya kimataifa zaendelea kuelekezwa Ukraine , ambako maandamano yamepamba moto .

Upande mmoja Urusi inaulaumu upinzani na kuutaka usitishe kile wanachokiita umwagaji damu .

Lakini waziri wa mambo ya nje wa Sweden , Carl Bildt, amesema Rais wa nchi hiyo Viktor Yanukovych, ndie anaepaswa kulaumiwa kwa vifo vya waandamaji 25 vilivyotokea.

Serikali ya Ukraine inapeleka wanajeshi wa angani huko Kiev kukabiliana na maandamano hayo yanayosambaa huku kukiwa na tisho la vikwazo vya kiuchumi kutoka umoja huo wa Ulaya.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.